1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aung San Su Kyi akutana na afisa wa serikali

11 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CoDC

YANGON

Mtetezi mkuu wa haki za binaadamu nchini Myanmar Aung San Suu Kyi leo amechukuliwa kutoka nyumbani kwake ambako amekuwa akizuiliwa kwa miaka 12 na kuepelekwa kukutana na maafisa wa utawala wa kijeshi wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa mashahidi amechukuliwa na kupelekwa katika kituo cha kijeshi kilioko karibu ambacho kwa kawaida hutumiwa kwa mikutano ya serikali.

Anatazamiwa kukutana na Waziri wa Kazi Aung Kyi ambaye ameteuliwa na utawala wa kijeshi kufanya mawasiliano naye kufuatia kuvunjwa kwa kutumia nguvu maandamano ya kudai demokrasia hapo mwezi wa Septemba ambapo watu kadhaa waliuwawa na wengine kujeruhiwa.