ATHENS:Wazima moto wadhibiti moto kwenye maeneo mengi | Habari za Ulimwengu | DW | 26.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ATHENS:Wazima moto wadhibiti moto kwenye maeneo mengi

Wazima moto nchini Ugiriki wamefanikiwa kudhibiti moto katika eneo la Kalyvia lililo katikati ya mji wa Athens na mji wa kale wa Sounion ulio kusini.Moto uliozuka nchini humo umesababisha vifo vya yapata watu 51 mpaka sasa na hali ya hatari kutangazwa na Waziri mkuu wa Ugiriki Costas Karamanlis.Maeneo mengine yaliyoshambuliwa na moto aidha yamedhibitiwa.Kwa mujibu wa idara ya kuzima moto juhudi zao zilifanikishwa na mvua kidogo iliyonyesha huku pepo kali zikipiga.

Upepo huo ulisababisha moto huo kusambaa katika maeneo mengi nchini humo tangu siku ya Ijumaa.

Maeneo ya milimani ya Peloponnese yaliyo kusini mwa nchi vilevile kisiwa cha Evia kilicho kaskazini mwa mji wa Athens yaliathirika zaidi.

Mapema hii leo miale ya moto ilifika katika vijiji vilivyo kilomita chache kutoka mji wa kale wa Olympia na mji wa Pyrgos.Hata hiyvo kulingana na idara ya kuzima moto mji wa Kalamata ulio kusini magharibi hauko hatarini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com