1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS:Chama tawala kimeshinda uchaguzi

17 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBP2

Chama kinachotawala cha kihafidhina cha waziri mkuu wa Ugiriki Costas Karamanlis cha New Democracy Party kimeshinda katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hapo jana.

Chama cha waziri mkuu huyo cha New Democracy Party kimepata asilimia 42 ya kura yaani viti 153 katika bunge lenye jumla ya viti 300.

Chama kikuu cha upinzani cha PASOK kinacho ongozwa na Giorgos Papandreou kimepata asilimia 38 ya kura au jumla ya viti 102.

Waziri mkuu Karamnlis aliitisha uchaguzi miezi sita mapema wakati hali ya uchumi wa nchi inandelea vizuri.

Lakini waziri mkuu huyo wa Ugiriki alilaumiwa vikali kuhusu alivyo shughulikia maafa ya mioto iliyoikumba nchi hiyo katika siku za hivi karibuni.