1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS: Barroso atembelea maeneo yaliyoteketezwa

1 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTf

Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso,ametembelea kwa helikopta maeneo yaliyoteketezwa kwa moto,kusini mwa Ugiriki. Barroso ameahidi kutoa misaada katika maeneo yaliyoathirika,ambako watu 64 walipoteza maisha yao katika moto na sehemu kubwa za misitu na mashamba zimeteketezwa.

Hii leo wakazi wa vijiji viwili walilazimika kukimbia moto unaoendelea kusababisha hasara kubwa.Barroso,baada ya kulitembelea eneo la Peloponnes pamoja na Waziri Mkuu wa Ugiriki Costas Karamanlis alisema,tatizo la Ugiriki ni tatizo la Ulaya na kile kilichoteketezwa kinapaswa kujengwa upya.

Siku ya Ijumaa,Umoja wa Ulaya uliarifu,Ugiriki huenda ikapewa msaada wa dharura wa Euro milioni 200 na msaada huo,unaweza kuongezwa baada ya kutathimini hasara iliyotokea.