1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASMARA : Makubaliano mengine ya amani Sudan

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2p

Serikali ya Sudan imesaini makubaliano ya amani na kundi la waasi kutoka mashariki mwa Sudan.

Makubaliano hayo yanakusudia kukomesha mzozo wa miaka 12 kati ya pande hizo mbili.Makubaliano hayo yametiwa saini huko Asmara mji mkuu wa Eritrea nchi ambayo imesaidia kufikiwa kwa makubaliano hayo ambayo yanajumuisha kushirikiana madaraka na mipangilio ya usalama kwa jimbo hilo la milima lilioko mashariki mwa Sudan.

Hayo ni makubaliano ya tatu ya amani kutiwa saini kati ya serikali ya Sudan na makundi ya waasi katika sehemu kadhaa za taifa hilo kubwa kabisa barani Afrika katika kipindi kisichozidi miaka miwili.