1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Askofu Mkuu Tutu atoa wito kwa Viongozi wa Kusini mwa Afrika kumshinikiza Rais Mugabe aachie madaraka.

24 Aprili 2008

Askofu Mkuu wa Afrika Kusini ambaye pia ni mshindi wa tunzo ya Amani ya Nobel, Desmond Tutu, ametoa wito kwa Viongozi wa nchi za Kusini mwa Afrika kumshinikiza rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kuachia madaraka.

https://p.dw.com/p/Do7f
Askofu Mkuu Desmond Tutu kulia akiwa na rais wa Kenya Mwai Kibaki.Picha: AP

Hii ni mara ya pili kwa Kiongozi huyo wa Kanisa kutoa wito kama huo tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo Machi 29.

Wito huo wa Askofu Tutu, ameutoa wakati akizungumza katika Mkutano wa masuala ya Elimu na Uongozi ulifanyika katika jimbo la Magharibi nchini humo.

Askofu Mkuu Tutu amesema Viongozi wa Kusini mwa Afrika hawawezi kuwavumilia viongozi wenye uchu wa madaraka na kwamba viongozi hao wanamambo mengi zaidi ya kuyashughulikia kama vile masuala ya njaa na ugonjwa sugu wa UKIMWI.

Amesema kuwa alitarajia kwamba Afrika Kusini ingeweza kumshawishi rais huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 84 asitaafu ili kulinda heshima yake.

Bado jamii ya Kimataifa inaendelea kumshinikiza Rais Mugabe ajiuzulu wakati chama chake cha ZANU-PF kikisisitiza kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi.

Kwa upande wake Chama Kikuu cha upindani -MDC, kinashikilia kwamba kimeshinda.

Wakati huohuo kazi ya kuhesabu kura tena inaendelea katika majimbo ishirini na tatu kati ya majimbo yote miambili na kumi.

Taarifa zinaeleza kuwa chama cha MDC kimepata ushindi katika jimbo la Zaka Magharibi huku chama Tawala cha ZAN -PF kikipata ushindi katika jimbo la Goromonzi Magharibi japo kuwa mpaka sasa hakuna mshindi yeyote wa urais aliyetangazwa.

Kwa upande mwingine Shirika la Kimataifa la kutetea haki za watoto limetoa wito kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedikto wa Kumi na Sita kufanya ziara nchini Zimbabwe kwa lengo la kumshawishi rais Robert Mugabe ambaye ni muumini mwa Kanisa hilo aweze kutuliza ghasia na kurejesha hali ya amani.

Katika barua yake ya wazi kwa Papa Benedikto wa Kumi na Sita, Shirika hilo la kutete haki za binadamu la Terre des Hommes (Ter de ZOM),lenye makazi yake Mjini Geneva, Uswis, lilitoa wito kwa Papa Benedikto kutia nguvu ya kuweza kumshinikiza rais Mugabe ili akubali kwamba nchini yake iko kwenye mgogoro na kuheshimu matakwa ya raia wa nchi hiyo.

Kiongozi wa Shirika la hilo Peter Muck, ambalo limeekuwa likishughulika na masuala ya Kimaendeleo nchini Zimbabwe, lilikuwa likirejea wito uliotolewa na madhahebu mbalimbali ya Kikristu nchini Zimbabwe ukimtaka Papa Benedikto wa Kumi na Sita kuchukua hatua fulani kuhusu hali ya Zimbabwe.

Katika taarifa yao ya pamoja viongozi hao wa Kanisa, alisema kuwa watu wamekuwa wakitekwa, kuteswa na hata kuuawa katika harakati zao la Kisiasa na kuzitaka nchi jirani za Kusini Magharibi, Umoja wa Nchi za Afrika na Umoja wa Mataifa kuingilia kati suala hilo.