1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASHGABAT. Zoenzi la kupiga kura lamalizika

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCT3

Zoezi la kupiga kura limekamilika nchini Turkmenikstan katika Asia ya kati kumchagua mrithi wa rais Saparmurat Niyazov aliyefariki.

Wagombea sita waliwania wadhfa huo wa rais kupitia chama kimoja tu cha kisiasa nchini humo.

Rais wa mpito Gurbanguli Berdymukhamenov anaaeungwa mkono na serikali anatarajiwa kunyakuwa ushindi.

Hii ni mara ya kwanza kwa nchi ya Turkmenkistan kuwashirikisha wagombezi wengi katika kinyang’anyiro cha urais.

Shirika la usalama na ushirikiano la bara ulaya limesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki.

Turkmenistan hapo awali ilikuwa jumuiya mojawapo katika utawala wa zamani wa Kisovieti na ina akiba kubwa ya gesi.

Nchi hiyo inapakana na Afghanistan na Iran.

Saparmurat Niyasov aliefariki Desemba mwaka jana aliiongoza nchi hiyo kimabavu.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kuanzia kesho.