1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA: Rugambarara ameadhibiwa kifungo cha miaka 11

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImQ

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa nchini Rwanda,imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 11 kwa meya wa zamani wa mji wa Bicumbi wa Rwanda, kuhusika na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa mauaji ya kiholela katika mwaka 1994.

Mhutu,Juvenal Rugambarara alie na umri wa miaka 48 amekubali makosa ya uhalifu kwa kukosa kuchukua hatua zilizohitajika,kuwaadhibu waliohusika na mauaji ya Watutsi katika mji wake. Jaji katika kupitisha uamuzi wake,amezingatia ukweli na majuto ya Rugambarara pamoja na msaada wa aina fulani aliyotoa kwa Watutsi.

Mahakama hiyo maalum ya Umoja wa Mataifa mjini Arusha,kaskazini mwa Tanzania ni mahakama kuu inayosikiliza kesi za washukiwa wakuu kuhusika na mauaji ya kiholela ya Watutsi na Wahutu wenye siasa za wastani wapatao takriban 800,000 nchini Rwanda katika mwaka 1994.