APEC YAITISHA HATUA JUU YA DURU YA DOHA | Habari za Ulimwengu | DW | 09.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

APEC YAITISHA HATUA JUU YA DURU YA DOHA

SYDNEY:

Viongozi wa nchi za Asia-Pacific au APEC wametoa mwito wa dharura kutaka maendeleo katika mazungumzo ya duru ya Doha yenye shabaha ya kuondoa vikwazo vya biashara ya bidhaa za kilimo na viwandani baina ya nchi tajiri na masikini.

Waziri mkuu wa Australia ,mwenyeji wa mkutano huo John Howerd aliwaambia waandishi habari kuwa viongozi hao 21 waliafiki pia kuimarisha muungano wa kiuchumi Alisema waziri mkuu wa Australia.

wa kimkoa na kusakas zaidi uwezekano wa kupanua eneo la biashara huru la Asia Pacific.

Viongozi hao halkadhalika waliafikiana hatua kadhaa zenye shabaha ya kupunguza ujoto ulimwenguni.

Waziri mkuu wa australia alisema:

„Ni hatua muhimu mno kuelekea makubaliano yenye maana sana ya kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayotambua haja ya kupiga hatua za maendeleo na za kiuchumi wa aina mbali mbali unaotoa matumaini tofauti.“

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com