1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan atoa wito wa kufanyika uchunguzi.

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyDZ

Nairobi.

Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusiana na uendeaji kinyume haki za binadamu nchini Kenya akisema kuwa mzozo wa kisiasa nchini humo umepindukia sasa mzozo juu ya matokeo ya uchaguzi. Wakati huo huo polisi nchini Kenya wanasema kuwa watu 19 wameuwawa katika mapigano ya kikabila katika mji wa Nakuru, na kufikisha idadi ya watu waliouwawa tangu Alhamis kufikia 45.

Ghasia hizo zimetokea licha ya matumaini ya maendeleo yanayopigwa baada ya rais Mwai Kibaki kukutana na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa mara ya kwanza siku ya Alhamis tangu kuanza kwa mzozo juu ya matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwezi wa Desemba.

Karibu watu 800 wameuwawa katika ghasia hizo nchini Kenya kufuatia mvutano kuhusu matokeo ya uchaguzi na zaidi ya watu laki mbili wamekimbia makaazi yao. Annan yuko nchini Kenya akifanya upatanishi wa jaribio la kupata suluhisho la kisiasa.