1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara.Waziri mkuu wa Uturuki aanguka kutokana na kushuka kwa sukari mwilini.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1v

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amekimbizwa hospitali mjini Ankara kwa matibabu, baada ya kuanguka na kupoteza fahamu.

Madaktari wamesema, waziri mkuu alikumbwa na matatizo ya kushuka kwa sukari mwilini, kulikosababishwa na funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyomsababisha kuchoka sana, baada ya safari nyingi za kikazi.

Baadae televisheni ilimuonyesha waziri mkuu Erdogan akizungumza na madaktari Hospitali.