ANKARA.waziri mkuu asema Uturuki itaendelea kufanya mageuzi | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA.waziri mkuu asema Uturuki itaendelea kufanya mageuzi

Wapinzani wakiwa nje ya Mahakama baada ya kupigwa nchini Zimbabwe

Wapinzani wakiwa nje ya Mahakama baada ya kupigwa nchini Zimbabwe

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema nchi yake itaendelea kufanya mageuzi licha ya pendekezo la kamisheni ya umoja wa ulaya la kusimamisha kwa muda mazungumzo kuhusu nchi yake kujiunga na umoja huo.

Pendekezo hilo lilifikiwa baada ya Uturuki kushindwa kufungua bandari zake kwa Cyprus ambayo ni mwanachama wa umoja wa ulaya.

Mawaziri wa mamabo ya nje wa nchi za umoja wa ulaya watakutana Desemba 11 kutoa uamuzi iwapo watazingatia pendekezo hilo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema amefurahishwa na hatua ya kuishinikiza Uturuki.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com