1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yaanza

25 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7D

Mpatanishi mkuu wa maswala ya nyuklia wa Iran Ali Larijani amewasili mjini Ankara nchini Uturuki kwa mazungumzo ya siku mbili na mkuu wa sera za nje wa umoja wa ulaya bwana Javier Solana.

Mazungumzo hayo yanalenga kutafuta njia za kutatua mzozo wa nyuklia wa Iran.

Bwana Larijani amesema kuwa nchi yake inataka mazungumzo yenye uhakika.

Umoja wa ulaya unataka kuishawishi Iran iachane na mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.

Tayari nchi 27 wanachama wa umoja wa ulaya zimepitisha azimio la kuweka vikwazo madhubuti dhidi ya Iran.