1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Balozi wa Uturuki wa Marekani arejeshwa nyumbani

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GZ

Uturuki imemrejesha nyumbani balozi wake wa Marekani kufuatia mzozo wa kidiplomasia kuhusu kura ya mauaji wa raia wa Armenia yanayoelezwa na Bunge la Congress la Marekani kuwa ya halaiki.Mauaji hayo yalitekelezwa Uturuki wakati wa utawala wa Ottoman.Uturuki inachukua hatua hiyo huku Ikulu ya Whitehouse iliyopinga kura iliyopigwa na kamati ya Bunge ya masuala ya kigeni ikijaribu kuipoza mwandani wake .Kamati hiyo ilipitisha azimio hilo hata baada ya Uturuki kuonya kuwa hatua hiyo huenda ikaathiri uhusiano kati yao.Spika wa Bunge Bi Nancy Pelosi anasisitiza kuwa bunge zima litapigia kura suala na sharti mauaji yasisahauliwe.

''Huenda tukio hilo ni la kitambo ila mauaji ya halaiki yanaendelea katika eneo la Darfur la Sudan na hivi karibuni yalitokea huko Rwanda.Kuna haja ya kulitaja na kushtumu mauaji ya halaiki kila yanapotokea.''

Uturuki kwa upande wake inakanusha hatua hiyo ya kuyaeleza mauaji hayo ya mwaka 1915-17 ya Warmenia kama ya halaiki.Hatua ya bunge kulipigia kura suala hilo huenda likasababisha Marekani kupoteza makao muhimu ya kijeshi nchini Uturuki. Rais Abdula Gul wa Uturuki alisema kuwa kura ya kamati hiyo haikubaliki na kuonya kuwa hatua zaidi huenda zikachukuliwa endapo bunge zima litaidhinisha hoja hiyo.

Yapata raia milioni 1.5 wa Armenia waliuawa katika kipindi cha mwaka 1915-17 wakati wa Utawala wa Ottoman nchini Uturuki.Kulingana na Armenia kampeni hiyo ililenga kusababisha mauaji na kurejeshwa kwa nguvu nchini mwao.

Uturuki kwa upande wake inakataa kurejesha uhusiano na jirani yake Armenia kwasababu ya juhudi zake za kutaka mauaji hayo kutambulika kimataifa kama ya halaiki