1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA.Baba mtakatifu atoa mwito wa kufanyika mdhalo baina ya waislamu na wakristo

29 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoT

Baba mtakatifu Benedikt wa 16 ametoa mwito wa kufanyika mdahalo wa dhati baina ya waislamu na wakristo.

Baba mtakatifu amesema hayo katika hotuba aliyotoa kwa mabalozi mjini Ankara kuanza ziara ya siku nne nchini Uturuki.

Amesema kuwa mdahalo huo unapaswa kuwa katika msingi wa ukweli na haja ya kufahamiana vizuri zaidi.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki pia ameonya matumizi ya nguvu kwa jina la dini.

Ziara ya baba mtakatifu nchini Uturuki imegubikwa na upinzani uliosababishwa na kauli aliyotoa nchini Ujerumani hivi karibuni ambapo alimkariri mfalme wa karne ya 14 aliyesema kuwa uislamu ni dini inayotumia ncha ya upanga.

Hata hivyo baba mtakatifu ameeleza kuwa aliyokariri hayawakilishi mtazamo wake binafsi.

Papa Benedikt wa 16 pia alikutana na kiongozi wa maimamu wa Uturuki Ali Bardakoglu ambapo alisisitiza umuhimu wa uhuru wa kuabudu.