Ankara: Majeshi ya Uturuki yakabiliana na waasi wa PKK. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ankara: Majeshi ya Uturuki yakabiliana na waasi wa PKK.

Wanajeshi watatu wa Uturuki wameuawa kwenye makabiliano kati ya majeshi na waasi wa chama cha Wakurdi cha PKK, mashariki ya nchi hiyo.

Wanamgambo watano wa chama hicho pia waliuawa.

Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi, askari wengine watano pia waliuawa kwenye makabiliano hayo katika jimbo la mashariki la Tunceli.

Wanajeshi kadhaa wameuawa mwaka huu kutokana na vita katika maeneo ya mashariki na kusini mashariki nchini Uturuki.

Serikali hiyo imepeleka majeshi yakakabiliane na uasi katika eneo hilo.

Chama cha PKK kimekuwa kikabiliana na majeshi ya Uturuki tangu mwaka 1984 kikiwania kujitenga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com