ANKARA: Gül kugombea urais nchini Uturuki | Habari za Ulimwengu | DW | 24.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA: Gül kugombea urais nchini Uturuki

Waziri wa mashuri ya kigeni wa Uturuki, Abdullah Gül, atagombea wadhifa wa urais nchini Uturuki.

Kiongozi huyo ana hakika ya kuwa rais wa nchi hiyo baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, kumtangaza kuwa mgombea wa chama chake cha AK atakayewania wadhifa huo.

Chama tawala cha AK cha Erdogan na Gül kina idadi kubwa ya wabunge katika bunge ambalo lina jukumu la kumchagua rais wa nchi.

Uamuzi huo ni wa kushangaza kwa sababu Erdogan alitarajiwa kugombea wadhifa huo kwa tiketi ya chama cha AK.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com