1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Bunge la Uturuki laidhinisha wapiga kura kumchagua rais moja kwa moja

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3W

Wabunge wa Uturuki wamepitisha mswada wa marekebisho ya katiba yanayopendekeza rais achaguliwe na wapiga kura.

Marekebisho hayo ni miongoni mwa marekebisho yaliyopangwa ya taratibu za uchaguzi.

Kwa mujibu wa spika wa bunge la Uturuki, wabunge mia tatu, sabini na sita kati ya wabunge mia tano na hamsini wameuunga mkono mswada huo ilhali wabunge hamsini na watano waliupinga.

Mapendekezo hayo yametolewa na chama tawala cha AKP kutanzua mzozo uliokuwepo bungeni kuhusu mtu anayepaswa kushikilia wadhifa wa urais.

Mapendekezo yote hayo yanapaswa kupitishwa bungeni kabla ya kuidhinishwa na Rais Ahmet Necdet.