ANKARA : Bunge la Uturuki laapishwa | Habari za Ulimwengu | DW | 05.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA : Bunge la Uturuki laapishwa

Bunge jipya la Uturuki limeapishwa kufuatia ushindi mkubwa wa chama chaKiislam cha AKP cha Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Jukumu la kwanza la bunge hilo litakuwa ni kumchaguwa rais mpya.Uteuzi uliopita wa chama hicho wa kutaka waziri wa mambo ya nje Abdullah Gul ashike wadhifa huo ulizusha maandamano makubwa ya watu wanaopinga kufungamanisha dini na taifa ambao wamekishutumu chama hicho kwa kutaka kudhoofisha utaratibu wa kutenganisha dini na taifa.

Chama hicho ambacho kimekana mizizi yake ya itikadi kali za Kiislam kinakanusha madai hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com