1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Angola na Tunesia uwanjani leo

Kombe la Afrika la mataifa likiendelea ,Angola inapambana na Tunisia leo na swali ni iwapo paa watachupa hadi duru ijayo ?

Kuparamia hatua kwa hatua kwa Angola kileleni mwa dimba la afrika kinaweza kukafikia kilele kipya hii leo katika changamoto ya paa hao na Tai wa carthage-Tunisia mjini Tamale.

Sare itatosha kuihakikishia Angola nafasi katika duru ijayo ya kutoana ya robo-finali.

Ni bafana Bafana-Afrika Kusini,wenyeji wa kombe lijalo la dunia 2010,waweeza kuinyima Angola tiketi ya robo-finali kutokana na tofauti ya magoli kwa kuilaza Senegal huko Kumasi.Afrika kusini itaomba dua paa wa angola-jirani zao, wanashindwa kwa mabao mengi na simba wa terange-Senegal leo.

Ikiwa Angola itasonga mbele leo na kutia fora kama ilivyofanya hadi sasa katika kinyan
‚ganyiro hiki cha kombe la Afrika baada ya kuitimua Senegal kwa mabao 3:1 jumapili iliopita, itaandika ukurasa mpya wa dimba kusini mwa Afrika.

Ikicheza kwa mara ya 4 tu katika finali za kombe la Afrika la mataifa ,hu uni mwaka wake kabla binafsi haikuandaa kombe lijalo la afrika 2010 nyumbani-mwaka wa kombe la dunia jirani Afrika kusini.

Angola utakumbuka iliondokea na pointi 1 katika kombe la 1996 lililochezwa Afrika kusini kabla haikuongeza pointi 1 miaka 2 baadae 1998 huko Burkina Faso.

Kuna sababu kwanini Angola inasonga mbele katika dimba la Afrika na imo kuvua lile joho la timu ambazo zinaitwa „pia zilishiriki“.Kwanza, yasuluhisha mizozo yake ya madai ya fedha na mapema nyumbani,pili haiwaruhusu wanasiasa kutia mkono wake katika dimba na tatu ina kocha muangola asiebadilishwa tangu 2003 Luis Oliveria Goncalves.

Sababu nyengine labda hakuna hata mchezaji mmoja wa angola anaetoka mojawapo ya klabu mashuhuri,lakini baada ya kombe hili la afrika sura hii yaonesha itabadilika:kwani, mshambulizi wa Angola:Manucho“ amefunga punde hivi mkataba wa miaka 3 na Manchester United ya uingereza.Muangola huyo tayari amepiga hodi mara 2 katika kombe hili la Afrika na kukaribishwa ndani.

Wachezaji wengine wanaotamba katika kikosi cha Angola ni msham,bulizi mwengine Flavio Amado pamoja pia na wachezaji wa kiungo akina Ze Kalanga, Gilberto na Maurito.

Hiki ndicho kikosi ambacho leo Tunisia,mabingwa 2004 nyumbani watakumbana nacho huko Tamale.lakini, hata Tunesia,imetamba katika kombe hili la Afrika na sioni njia nao kuregeza kamba mbele ya Angola.

Tunisia ilinusurika kuzamishwa marekebu yao na mizinga ya mfululizo ya Senegal na ikatoka nyuma kusawazisha mabao 2 na kuondoka sare na simba wa Terange.Baadae, tunisia ikawaelemea chipukizi wa bafana Bafana na kuwakandika mabao 3-1.

Kocha wao mfaransa Roger Lemerre kwa mara ya kwanza leo ataweza kumteremsha uwanjani stadi wao Amine Chermiti,mshambulizi hatari kabisa na mchanga kutoka klabu bingwa ya Afrika Etoile du sahel.Chermiti anakodolewa sasa macho na klabu za Ufaransa na Uswisi.

Pamoja na Chermiti kuna dos Santos, mtunesia wa asilio ya Brazil aliewafumania Bafana Bafana majuzi kwa mabao yake 2.

Isitoshe, mbali na Dos Santos,walinzi Radhi na Jaidi pamoja na Karim Hagui na hata pia wachezaji wa kiungo akina Jouhar Mnari na Mehdi Nafti ni kikosi kinachotokana na ile timu ilioilaza Morocco na kutawazwa nyumbani mabingwa wa Afrika 2004.

Baada ya kutimuliwa Morocco,Tunesia na Misri,ni timu 2 pekee bado zinazopepea bendera ya Afrika ya kaskazini katika kombe hili la dunia mbele ya madume wa Afrika magharibi:Tembo wa Ivory Coast,Black Stars-Ghana, Simba wa nyika Kameroun na Guinea.

 • Tarehe 30.01.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Czqx
 • Tarehe 30.01.2008
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/Czqx

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com