1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angela Merkel ashutumiwa kwa sera zake za Ulaya

26 Agosti 2011

Angela Merkel amelazimika kusikia sasa shutuma kutoka kwa watu ambao wako upande wake kuhusiana na sera zake za kisiasa katika Ulaya.

https://p.dw.com/p/12ORq
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye ameshutumiwa na viongozi kutoka chama chake cha CDU kuhusu sera zake za Ulaya.Picha: dapd

Angela Merkel amelazimika sasa kusikia shutuma kutoka kwa watu wa ngazi yake kutokana na sera zake za kisiasa katika Ulaya. Hata kansela wa zamani Helmut Kohl na rais wa Ujerumani Christian Wulff wamemtupia lawama kansela , hususan kukiwa na hisia kuwa wananchi wamepata ushindi kupitia katika vyombo vya habari. Lakini hisia hizi kwa hakika ni sehemu tu.

Ni matumani kwamba kansela Merkel amepumzika vya kutoka katika likizo yake. Kwa sababu mara tu aliporejea amepambana na vichwa vya habari katika vyombo vya habari, vikisema ; Helmut Kohl, wito muhimu kwa Merkel, tunapaswa kujihadhari, kwamba hatujafanikiwa kwa kila kitu. Limeandika hivyo gazeti linaloonekana kuwa la udaku la Bild, likiwa na wasomaji zaidi ya milioni moja. Kisha linasisitiza gazeti ambalo huangaliwa kuwa ni makini zaidi la Süddeutsche Zeitung, likiwa na kichwa cha habari, Kohl : Sera ya mambo ya kigeni ya Merkel haina dira.

Kwa kweli Helmut Kohl alifanya mahojiano na gazeti lenye hadha ya juu la International Politik. Katika mahojiano hayo kansela wa zamani Kohl amehoji kuhusiana na uamuzi wa kukataa vita vya Iraq mwaka 2003 uamuzi uliofanywa na kansela wa zamani Gerhard Schröder na Ujerumani kutopiga kura katika uamuzi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa katika azimio kuhusu Libya mwaka huu. Ujerumani imepoteza dira yake?. Mwanasiasa huyo mzoefu wa masuala ya kigeni na ambaye alipata mafanikio makubwa katika wakati wake anajibu. Kwa bahati mbaya tunapaswa kusema hivyo. Na anatoa wito wa kurejea katika hali ya zamani.

Bekanntgabe des Roland-Berger-Preises für Menschenwürde 2010
Kansela wa zamani Helmut Kohl, amemkosoa kansela wa sasa kutokana na sera zake kwa Ulaya.Picha: AP

Ukosoaji wa Kohl bila shaka unamgusa pia mrithi wake Angela Merkel, licha ya kuwa hakumtaja moja kwa moja. Amekosoa zaidi kansela wa zamani utawala uliofuatia wa chama cha SPD na kijani. Anaushutumu utawala huo kwa hali ya sasa ya madeni katika eneo la mataifa ya euro. Wameiingiza Ugiriki katika eneo la euro bila ya kuangalia matumizi yake katika bajeti pamoja na viwango vya uthabiti vya umoja wa sarafu wa umoja wa Ulaya. Shutuma za moja kwa moja dhidi ya utawala wa Merkel ni kwamba haufahamu ni ushauri gani uufuate , ama kitu gani kingine ufanye.

Hilo ndio tatizo kubwa la utawala wa Angela Merkel hivi leo. Kuna ukosoaji mkubwa juu ya jinsi anavyolishughulikia suala la mzozo wa eneo la euro, lakini , mapendekezo mbadala , hadi sasa yanayokuja anayapinga. Serikali ya Ujerumani kama washirika wake wa Ulaya , haikujiweka kuwa mfano wa mbele, kwa kuwa kuna kitu kama umoja wa sarafu wa umoja wa Ulaya bado haupo. Lakini pamoja na hayo , uamuzi kwa kiasi kikubwa ni mbovu.

Mwandishi : Peter Stützle / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo