1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANC kinaongoza katika uchaguzi Africa Kusini

Mwandishi Saumu Mwasimba23 Aprili 2009

Cope kiko nafasi ya Tatu kinyume na ilivyotarajiwa

https://p.dw.com/p/HcWk
Wafuasi wa chama Tawala cha ANC wajiandaa kusherekea ushindi''Picha: picture-alliance/ dpa

Dalili zote nchini Africa Kusini zinaonyesha kwamba Jacob Zuma kiongozi wa chama tawala cha ANC yuko katika njia ya kuelekea kuwa rais wa taifa hilo wiki chache baada ya kushinda ya rushwa iliyokuwa inamkabili.

Matokeo ya awali yanaonyesha kwamba chama cha African Nation Congress kimeshajizolea aslimia 64 ya kura zilizohesabiwa hali ambayo inayadidimiza matumaini ya wapinzani wao kutoka chama cha COPE kilichoundwa na wanachama waliojitenga na ANC kwamba huenda wakawapa upinzani mkali hali ambayo haijatokea tangu kumalizika enzi ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

Südafrikas größte Oppositionspartei verspricht Wandel - Helen Zille
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) Helen ZillePicha: picture-alliance / dpa

Chama cha COPE kiko katika nafasi ya tatu kikijipatia asilimia 7.7 ya kura katika matokeo ya awali ya kura zilizohesabiwa.Upinzani mkali hata hivyo umetoka katika chama cha Demokratic Alliance kinachoongozwa na mwanamama wa kizungu ambacho kimejipatia asilimia 19.3.Ibrahim Fakir ni afisa kutoka tasisi ya uchaguzi nchini Afrika kusini.

''Nafikiri mshindi katika kinyang'anyiro hiki ameshatambulika bila shaka inaonyesha ANC kitashinda na nafikiri pia kinaweza kupata asilimia 65 ingawa kiwango hicho ni kidogo kwa asilimia 2 ikilinganishwa na matokeo ya uchaguzi uliopita.''

Ibrahim pia anasema juu ya kwamba ANC kinaongoza jambo la kufurahisha ni kwamba mara hii chama hicho kinakabiliwa na kibarua kufikia thuluthi tatu ya viti bungeni. Vyama vya upinzani vinatarajia angalau kukinyima nafasi chama cha ANC ya kupata wingi huo wa thuluthi mbili katika bunge la viti 400 wingi ambao unawapa uwezo wa kubadili katiba.Hata hivyo hali ambayo imejitokeza ni kwamba bado ni mapema mno kubashiri ikiwa chama tawala kitashindwa kupata wingi huo.

Msemaji wa chama hicho tawala cha ANC Jessie Duarte amesema kwamba dalili zote zinaonyesha chama chake kimeshinda uchaguzi huo kwa wingi mkubwa lakini hakitaki kujitangazia ushindi kwa sasa ingawa matokea ya awali yanaonesha ushindi mkubwa kwa chama hicho.Ameongeza kusema kwamba ANC kitajitangaza mshindi wakati asilimia 90 ya kura zute zikiwa zimeshahesabiwa.

Kwa upande mwinghine kiongozi wa zamani wa upinzani Tony Leone amesema kwamba anafikiria hadi sasa chama hicho tawala hakijapata wingi wa thuluthi mbili ingawa huenda kinakaribia kufikia huko.Hadi sasa tume ya uchaguzi imetangaza kwamba kura zaidi ya milioni tatu zimehshahesabiwa na shughuli hiyo bado inaendelea katika vituo mbali mbali.

Zaidi ya watu 23 millioni walijiandikisha kupiga kura katika uchaguzi uliofanyika jana uchaguzi ambao ni wa nne tangu kumalizika rasmi enzi ya ubaguzi wa rangi mwaka 1994.Tume hiyo ya uchaguzi haijatangaza lakini idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura lakini ilitabiri kwamba watu wengi walijitokeza.

Courtne Simpson afisa wa tume huru ya uchaguzi anasema-

''Nafikiri ni jambo la kupendeza kwamba watu walijitokeza,tunabidi kama tume ya uchaguzi ya kitaifa na mikoani kuipoingeza hatua hiyo kama ya kidemokrasia''

Chama cha Demokratic Alliance kinaongoza katika mkoa wa Cape Magharibi kwa asilimia 55 ya kura mkoa ambao ulikuwa ukidhibitiwa na chama cha ANC.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa hapo kesho ijumaa ingawa tayari.

Mwandishi Saumu Mwasimba AFPE

Mhaririri Mohd Abdul Rahman.