1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANBAR:Idadi ya majeshi ya Marekani kupunguzwa Iraq

Rais George Bush wa Marekani ameelezea mipango ya kupunguza majeshi ya nchi hiyo huko Iraq.

Alisema hayo hapo jana mjini Anbar Iraq katika ziara yake ya ghafla.Rais Bush alikutana na makamanda wa juu wa jeshi hilo pamoja na w ashauri wa wengine ambao walimuelezea kazi kubwa majeshi hayo inayokumbana nayo.

Rais Bush hata hivyo alielezea kubadilika kwa hali kwa hali ya maisha katika jimbo hilo.

Rais Bush alifanya ziara hiyo ya ghafla akiwa njiani kuelekea Sydney Australia kwenye mkutano wa wakuu wa Asia na Pacific.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Browon ameelezea uamuzi wa nchi hiyo kuyaondoa majeshi yake nchini Iraq.

Kiasi cha wanajeshi 500 wa Uingereza waliyokuwa katika mji wa kusini wa Basra wamejiondoa na kuweka kambi nje kidogo ya mji huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com