1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN: Mfalme Abdullah wa Jordan amuonya Condoleezza Rice

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaP

Mfalme Abdullah wa Jordan amemuonya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice kwamba kushindwa kuyaharakisha mazungumzo ya kutafuta amani ya Mashariki ya Kati kunaweza kusababisha machafuko mabaya zaidi.

Maofisa wa Jordan wamesema mfamle Abdullah amefuruhishwa na hatua ya Marekani kujihusisha katika juhudi za kutafuta amani na akasema atazishawishi pande husika ili Marekani ichukue usukani katika juhudi za kutafuta amani ya Mashariki ya Kati.

Hapo jana Condoleezza Rice alizungumza na mfalme Abdullah wa Jordan mjini Amman kuhusu njia za kuyafufua tena mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.

Jana pia Bi Condoleezza Rice alimuahidi rais wa Palestina Mahmoud Abbas kwamba Marekani itamsaidia kufikia kuundwa kwa taifa huru la Wapalestina na akasema atauharakisha mpango wa amani ya Mashariki ya Kati uliokwama.

Hata hivyo Condoleezza akiwa katika ziara yake ya nane katika eneo hilo, hakutoa maelezo zaidi vipi Marekani itakavyoziharakisha juhudi hizo za kutafuta amani.