1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN : al- Maliki awasili Jordan

29 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCoM

Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al Maliki amewasili nchini Jordan kwa mazungumzo na Rais George W Bush wa Marekani.

Bush anatazamiwa kuwasili nchini humo leo hii akitokea Latvia kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO.

Mazungumzo kati ya viongozi hao yanatazamiwa kulenga njia za kuzuwiya kuharibika zaidi kwa hali ya usalama nchini Iraq.Kabla ya kuelekea nchini Jordan kwa mkutano huo ambao pia utamjumuisha Mfalme Abddallah wa Jordan Bush alisema.

Mapema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limeidhinisha mamlaka mpya kuruhusu kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na Marekani kuendelea kubakia nchini Iraq kwa miezi mengine 12 wakati Iraq ikiunda vikosi vyake yenyewe.Kikosi hicho cha kimataifa kitaendelea kubakia nchini humo hadi mwishoni mwa mwaka 2007.

Marekani ina takriban wanajeshi 150,000 nchini Iraq.