1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amani ya Mashariki ya Kati yapata msukumo mpya

Mwadzaya, Thelma14 Julai 2008

Mataifa 43 yakiwemo mataifa ya Kiarabu na Israel yameafikiana kushirikiana ili kuhakikisha silaha za maangamizi makubwa zinatokomezwa katika eneo la mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/Ebj9
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy(kati) na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas(kushoto) and Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert huko ParisPicha: AP



Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuanzishwa rasmi kwa Umoja wa mataifa ya Meditarana.Jumuiya hiyo ilizinduliwa rasmi mjini Paris na mwenyeji wa kikao hicho Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy aliyefurahishwa sana na hatua hiyo.


Kikao hicho kiliwaleta pamoja viongozi kutoka Ulaya,Mashariki ya kati vilevile Afrika.Katika kauli yao ya pamoja kabla kukamilisha kikao hicho wawakilishi wa nchi hizo waliafikiana kutokomeza silaha za maangamizi makubwa katika eneo la mashariki ya kati.Wadau wa Mashariki ya kati waliafikiana na kauli hizo.


Israel kwa upande wake inaamini kuwa suluhu inaweza kupatikana na mataifa mawili kuundwa na kuishi pamoja kwa amani.


Kauli hiyo pia inakashifu ugaidi wa aina yoyote ile na kutangaza kuanzishwa kwa miradi sita inayojumuisha kuanzishwa kwa chuo kikuu cha pamoja,kurahisisha usafiri kwa wanafunzi,kupinga uchafuzi wa bahari ya Meditarana pamoja na kuyapa kipa umbele matumizi ya nishati ya jua.