1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

al-Sadr aionya serikali ya Irak

20 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dl3f

Baghdad:

Kiongozi wa kishia nchini Irak Moqtada al- Sadr ametishia "vita kamili" na serikali ya Irak endapo haitositisha harakati za kijeshi dhidi ya wafuasi wake. al-Sadr alisema anaipa serikali "onyo la mwisho" na kuitaka ifuate mkondo wa amani. Taarifa ya kiongozi huyo imetolewa katika wakati ambao majeshi ya Irak yakisaidiwa na yale ya Marekani na Uingereza yakipambana na jeshi la Mehdi la wafuasi wa al- Sadr mjini Baghdad na katika miji ya kusini ya Nasiriya na Basra. Taarifa za mashirika ya habari zinasema mapigano huko Basra yalikua makubwa kabisa tangu mwezi uliopita, wakati jaribio la serikali la kuwapokonya silaha wapiganaji hao na wanamgambo wengine katika mji huo wa bandari kusini mwa nchi hiyo, liliposhindwa.