1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajali kwenye mgodi wa almasi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

5 Aprili 2007

Kumetokea ajali ya mporomoko wa udongo kwenye mgodi wa almasi unaopatikana mjini Mbuji-Mayi jimboni Kassai mashariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/CHGr
Mfanyakazi wa mgodi wa almasi mashariki mwa Kongo.
Mfanyakazi wa mgodi wa almasi mashariki mwa Kongo.Picha: AP

Watu kumi na moja tayari wamefariki na wengine wengi wameendelea kubaki chini ya udongo. Wakati huo huo, jeshi la Umoja wa Mataifa MONUC inasema kwamba watu watatu wameuwawa, wengine wengi walikamatwa kwa nguvu na wengine 65.000 wamekimbia makaazi yao jimboni Kivu ya kusini kufuatia mashambulio ya mara kwa mara ya wana mgambo wa kihutu wa jeshi la zamani la Rwanda wanaopatikana mashariki mwa Kongo.

Mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo ametuletea taarifa kamili.