Ahmedinejad athibitishwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi. | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.08.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ahmedinejad athibitishwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi.

Maandamano ya baada ya uchaguzi mkuu wa rais nchini Iran yameitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mkubwa wa kisiasa tangu kuundwa kwa jamhuri hiyo ya Kiislamu miaka 30 iliyopita.

default

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad, akiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Malaysia.

Maandamano ya baada ya uchaguzi mkuu wa rais nchini Iran yameitumbukiza nchi hiyo katika mzozo mkubwa wa kisiasa tangu kuundwa kwa jamhuri hiyo ya Kiislamu miaka 30 iliyopita. Leo kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei amemthibitisha rasmi rais Mahmoud Ahmedinejad kuwa mshindi wa uchaguzi huo. Tarehe 5 August siku ya Jumatano rais huyo ataapishwa kuchukua rasmi madaraka kwa kipindi cha pili. Siku ya Jumamosi August mosi watu wanaokadiriwa kufikia 100 walifikishwa mbele ya mahakama mjini Tehran kwa kushiriki katika maandano na kuikosoa serikali.

Yule aliyetarajia ama pengine wachache waliotumai kuwa matokeo yaliyotangazwa na maafisa wa tume ya uchaguzi nchini Iran yangetangazwa kinyume chake, hao wanapaswa kuelimishwa zaidi.Kiongozi wa sasa na mshindi wa uchaguzi huo Mahmoud Ahmedinejad amethibitishwa na kiongozi wa juu wa kidini Ayattollah Ali Khamenei na baada hapo bunge la nchi hiyo katika muda wa siku mbili zijazo litamthibitisha pia kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Kimtazamo ni kwamba kiongozi huyo amesimamia yale anayoyataka kama ilivyokuwa katika uchaguzi, kwamba hapo Juni 12 uchaguzi huo umefanyika kwa haki na kama ilivyo nchini mwake ama kimataifa Ahmedinejad ambaye anaonekana kuwa ni kiongozi mwenye utata, alipata wingi mkubwa kupita kiasi.

Kwa upande wa upinzani na wapiga kura ambao hawakuridhika hatua ya kuthibitishwa Ahmadinejad madarakani inaendelea kuwa ni pigo kubwa kwao.

Wiki kadha za maandamano hazikuleta mabadiliko yoyote. Mbinyo kutoka kwa jeshi la usalama nchini humo ulikuwa mkubwa. Maandamano yalipigwa marufuku na kuvunjwa kwa nguvu , pamoja na hayo lakini imethibitika kuwa viongozi kadha wa vyama na maelfu ya watu walioshiriki katika maandamano walikamatwa na mamia kati yao walifikishwa mbele ya mahakama mwishoni mwa juma.

Na hii ni njia mojawapo ya kuwaangalia wapinzani kuwa wakati Ahmedinejad anaingia katika kipindi chake cha pili cha utawala , wapinzani wake watakuwa kama wapiganaji , vibaraka wa mataifa ya kigeni na wapinzani wa jamhuri hiyo ya Kiislamu. Atakayeamini ni yule tu anayetaka. Kwa sababu kwakweli wameweza kuleta mbinyo, lakini wameshindwa kuleta ushahidi wa pamoja wa uhalifu uliotokea , ili kuweza kuthibitishwa, kwamba mgombea wa upinzani Mousavi pamoja na marais wawili wa zamani Khatami na Rafsanjani ambao kabla ya uchaguzi walikuwa pamoja na kushindwa kuzuwia kuchaguliwa tena kwa rais Ahmedinejad.

Kile ambacho wapigakura wamekionyesha kupitia demokrasia kimezuiwa na mahakama ya jinai mjini Tehran.

Wanasiasa hao watatu kwa kweli walitaka kumharibia Khamenei. Na kwamba inaonyesha kuwa kwa njia yoyote ile wanataka kupambana na mfumo wa jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Wakati lakini wanasiasa hao watatu watakapofikishwa mahakamani , itaonyesha kwamba watawala hawako katika hali ya utulivu. Wanatambua kama ilivyo kwa kila mtu nchini humo kuwa maandamano ya wiki zilizopita hayakupangwa kutoka nje ili kujaribu kuiangusha serikali, badala yake msisitizo ulikuwa kutokana na kutoridhika. Kundi kubwa la wananchi wanakubali matokeo ya uchaguzi, lakini hali ya mambo nchini humo kwa kiasi kikubwa si ya kuridhisha.

Mwandishi ;Peter Philipp/ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri Mohamed Abdul-Rahman.

►◄

 • Tarehe 03.08.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/J2sD
 • Tarehe 03.08.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/J2sD

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com