1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ahamdinejad anakabiliwa na changamoto nyingi

5 Agosti 2009

ras mpya ni wa zamani Iran.

https://p.dw.com/p/J4CG
Ahmadinejad,Picha: AP

►Akitolewa maanani na nchi za magharibi kwa siasa zake kali na akikabiliwa na upinzani mkali nchini Iran kwa "mizengwe katika uchaguzi wa Juni 12, mwaka huu,Rais Ahmadinejad alieapishwa rasmii hiii leo ameonesha bado ana uwezo wa kuwatia munda mahasimu wake.Hatahivyo, kuchaguliwa kwake kwa kipindi cha pili cha urais kuanzia leo hakujafanyika bila mhanga.

Turufu kubwa katika maisha ya kisiasa ya rais Ahmadinejad,mwenye umri wa miaka 53 ni kwa wapinzanii wake kumdharau uwezo wake.Hii imempa mwanya na pumzi zaidi kuiimarisha madaraka yake.Hatahivyo, mara hii amekumbana na changamoto kali ya upinzani kutoka ndani ya Iran ,upinzani usiowahi kuonekana tangu miaka 30 iliopita.Matokeo ya uchaguzi ambayo wapinzani wsake wakubwa wapendamgeuzi wenye sera za wastanii Mirhossein Mousavi na Mehdi Karoubi wamedai yametokana na mizengwe,yaliongoza katika machafuko makubwa na kuzusha ufa mkubwa tangu katika safu ya maayatollah wa Jamhuri hii ya kiislamu ya Iran hata viongozi maarufu wa kisiasa.

Hii si mara ya kwanza kwa Ahmadinejad,kupindua juu chini vile ilivyobashiriwa kutokea.Mlinzi huyu wa zamani wa mapinduzi ,alikuwa mtu asiefahamiika alipoteuliwa diwani wa mji mkuu Teheran 2003 na hata hakuwa maarufu alipomshinda raiis wa zamani Akbar Hashemi rafsanjani katika changamoto ya wao 2 kwenye uchaguzi wa 2005.

Katika kipindi chake cha kwanza cha urais,Ahmadinejad aligonga vichwa vya habari ulimwenguni kwa matamshi yake makalii dhidi ya marekani na Israel,msimamo wake usiotetereka katika kutetea mradi wa kinukliia wa IIran na kuendelea kubisha kutokea msiba wa kuhilikishwamayahudi-holocaust.

Akiwa amezaliwa katika kijiji kidogo cha Aradan,maiili 60 kusini magharibi mwa mji mkuu Teheran,alihamia mji mkuu na familiia yake akiwa bado mtoto.Alijifunza uhandisi na wakati fulani alichukua kazi ya uwalimu na mwengine ya utawala.kampeni yake alielekeza kuupiga vita umasiikini,dhulma katika jamii na kugawa upya utajiri nchini Iran kuleta usawa.Aliahidi kuutumia utajirii wa mafuta ya Iran kunufaisha kila ukoo katika nchi hii ya wakaazii milioni 70.

Wapinzani wake na baadhi ya wanaomuungamkono wakihafidhina, wamemkosoa jinsi alivyouharibu uchumi wa Iran wenye kuegemea petroli.Mapato makubwa ya dala za mafuta wanadai ameyafisidi.

sasa mwanasiasa huyu mwenye imani ya imam mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, sasa ana njia yaenye mabonde mengi.Kinyanganyiro cha madaraka nchini Iran kitamwekea pingamizi katika kuyatatua matatizo ya kiuchumi ya Iran pamoja kukabili shinikizo kubwa kuhusu mradi wake wa kinuklia.

Katika hotuba yake leo baada ya kuapishwa, Ahamdinejad alisema uongozi wa wanazouni wa kiislamu nchini Iran ,nii imara vya kutosha kupambana na changamoto tangu za ndanii hata za nje ya Iran .

Mwandishi:Ramadhan Ali/RTRE

Mhariri:M.Abd