1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika yahitaji dola milioni 500 kukabiiana na ongezeko la bei za vyakula

11 Machi 2008

Umoja wa Mataifa hapo jana umetowa wito wa kupatiwa dola milioni 500 kwa ajili ya mahitaji ya dharura ya Afrika kukabiliana na ongezeko la bei za vyakula duniani.

https://p.dw.com/p/DMMZ

NEW YORK

Hali hiyó inaweza kukwamisha malengo ya maendeleo na juhudi za kupambana na umaskini katika nchi za kimaskini.

Wito huo umetolewa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kundi la Kamati ya Uendeshaji ya Afrika inayokutana kuchambuwa maendeleo katika kuweka malengo ya kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milinia ikiwa ni pamoja na idadi ya watu wanaoishi kwa kutumia pungufu ya dola moja kwa siku ifikapo mwaka 2015.

Malengo ya Maendeleo ya Milinia yaliozinduliwa hapo mwaka 2000 hivi sasa yako nusu njia lakini ni mataifa machache tu ya Afrika yamefanikisha baadhi ya malengo hayo katika kutokomeza umaskini na njaa,elimu ya msingi kwa wote, usawa wa kijinsia,kupunguza vifo vya watoto wadogo na kuboresha afya ya uzazi pamoja na kuzuwiya kuenea kwa virusi vya HIV na UKIMWI ifikapo mwaka 2015 .

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-mooon hapo jana amesema anapanga kuandaa kwa pamoja mkutano wa ngazi ya juu hapo mwezi wa Septemba juu ya kuzorota kwa utekelezaji wa Malemngo ya Maendeleo ya Milinia ya kupungza umaskini hususan barani Afrika.