1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Abdu Said Mtullya12 Aprili 2013

Wiki hii gazeti la"Berliner Zeitung" limeandika juu ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa nne wa jamhuri ya Kenya. Magazeti ya Ujerumani wiki hii pia yameandika juu ya biashara ya simu za mkononi barani Afrika

https://p.dw.com/p/18F7s
Uhuru Kenyatta aapishwa kuwa Rais.
Uhuru Kenyatta aapishwa kuwa RaisPicha: Reuters

Gazeti la Süddeutsche Zeitung linasema katika makala yake kwamba hakuna sehemu nyingine yoyote duniani ambako biashara ya simu za mkononi inastawi kwa haraka kama barani Afrika.

Kenyatta aapishwa :

Gazeti la" Berliner Zeitung" limeandika juu ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa nne wa jamhuri ya Kenya.Gazeti hilo limeanza makala yake kwa kusema kuwa Uhuru Kenyatta ameahidi kuleta maridhiano nchini Kenya.Lakini gazeti hilo linatilia maanani kwamba Kenya imegawanyika.

Linaeleza kuwa katika hotuba yake Kenyatta alizungumuzia juu ya umuhimu wa kuleta maridhiano kwa kwa kuahidi kuwatumikia Wakenya wote.Lakini ukweli unabakia pale pale kwamba alichaguliwa kwa kura nyingi za watu wa kabila lake la Wakikuyu. Pia aliungwa mkono na kabila la Kalenjini la makamu wake William Ruto.Gazeti la "Berliner Zeitung"linasema mgombea mwingine, Raila Odinga alipigiwa kura na watu wa kabila lake la Waluo.

Odinga hakuonekana kwenye sherehe ya kuapishwa Rais

Gazeti la"Berliner Zeitung" linasema Odinga alikubali kushindwa baada ya Mahakama ya Juu ya Kenya kuamua kwamba Kenyatta alishinda uchaguzi kwa haki.Hata hivyo gazeti hilo limeripoti kwamba Odinga hakuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa nne wa jamhuri ya Kenya.Gazeti la "Süddeutsche Zeitung"pia limeandika juu ya Kenya kwa kutilia maanani kwamba hali ya kawaida imerejea katika nchi hiyo. Lakini gazeti hilo pia limeandika juu ya Rais wa Sudan,Omar Bashir ambaye hakuenda kwenye sherehe ingawa alialikwa.

Kenya's Prime Minister and presidential candidate Raila Odinga gives an interview to AFP on January 14, 2013, in his office in Nairobi. Kenya is less than two months away from the first presidential elections since deadly post-poll violence five years ago. While two main candidates -- Uhuru Kenyatta and Raila Odinga -- dominate the race, all six candidates have potential influence, especially if voting goes to a second round run off after the March 4 vote. AFP PHOTO/SIMON MAINA (Photo credit should read SIMON MAINA/AFP/Getty Images)
Raila Odinga aliyeshindwa katika uchaguziPicha: Getty Images/AFP


Linasema katika taarifa yake kwamba, hadi dakika za mwisho shingo za watu zilikuwa juu kuangalia iwapo Rais Bashir angelihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Kenyatta Hata hivyo gazeti la "Süddeutsche" limearifu kwamba Omar Bashir aliahirisha safari ya kuenda Kenya.

Gazeti hilo pia limeandika juu ya biashara ya simu za mkononi.Gazeti hilo linasema biashara hiyo inastawi bila ya kifani duniani..Linaeleza kuwa kuwa simu za mkononi zinatumiwa pia kwa ajili ya kutumia fedha Kwa mfano "M pesa" sasa ina wateja zaidi ya milioni 20 nchini Kenya. Hiyo ni nusu ya idadi ya wananchi wa Kenya. Biashara ya simu za mkononi imeongezeka kutoka wateja milioni 90 hadi 475 katika kipindi cha miaka saba katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Biashara ya mitumba :

Biashara ya mitumba pia inazidi kustawi barani Afrika. Lakini ni nani hasa ananufaika zaidi? Gazeti la"Kölner Stadt-Anzeiger",limeripoti juu ya mchezo wa tamthilia kuhusu mitumba. Limearifu kwamba wasanii walioshiriki katika mchezo huo ulioigizwa katika mji wa Cologne pia walitoka,Nigeria,Kenya na Tanzania. Gazeti la "Kölner Stadt-Anzeiger " limemnukuu msanii mmoja kutoka Ujerumani akiwaambia watu kwamba alifanya ziara katika nchi moja ya Afrika mashariki ambako aliwaona watu karibu laki tano kila siku wakinunua nguo za wazungu waliokufa.

Gazeti la"Kölner Stadt Anzeiger " linasema kwamba watu wanaostahili kupata mitumba hawanufaiki sana na nguo hizo.Gazeti hilo linaarifu kwamba mitumba ambayo ni mizuri inapelekwa katika nchi za Mashariki ya Kati.Mchezo wa tamthlia juu ya mitumba ulionyesha wapi mitumba inauzwa, bei na wafanyabiashara wa nguo hizo.

Jenerali Nzeyimana akamatwa ?

Gazeti la"die tageszeitung" limeripoti juu ya kukamatwa kwa kamanda wa wanamgambo wa kihutu FDLR jenerali Stanislas Nzeyimana. Kwa mujibu wa gazeti hilo, jenerali Nzeyimana alikamtwa nchini Tanzania na kupelekwa Rwanda.

Lakini habari hizo hazithibitishwa na Tanzania wala Rwanda.

Mwandishi: Mtullya Abdu/ Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Khelef