1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Adiss Ababa.Viongozi wa Kiafrika wakutana kuzungumzia kuhusu Ivory Coast.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD23

Viongozi wapatao kumi wa kiafrika wamepangiwa kukutana katika makao makuu ya Umoja wa Afrika Adiss Ababa hii leo, kuzungumzia mizozo ya kisiasa nchini Ivory Coast.

Mkutano huo wa Viongozi unaitishwa kwa kikao cha baraza la amani na usalama la umoja wa Afrika, kuandaa msimamo wa taasisi hiyo ya kiafrika kwa ajili ya mkutano wa umoja wa mataifa, utakaozungumzia hali nchini Ivory coast.

Jumamosi iliyopita, mjumbe wa umoja wa mataifa anaesimamia uchaguzi nchini Ivory Coast, Gerard Stoudman alisema, uchaguzi unaoakhirishwa kila mara katika nchi hiyo iliyogawika kwa sababu ya vita, utaakhirishwa tena kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuitishwa kabla ya October mwakani.