1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Wanadiplomasia 6 wa Norway watimuliwa

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVF

Serikali ya Ethiopia imewaamrisha wanadiplomasia sita wa Norway kuondoka nchini humo kufikia septemba 15.

Serikali hiyo imesema inawatimua wanadiplomasia hao kufuatia kutoridhishwa na tabia za Norway katika eneo hilo la Pembe ya Afrika.Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Norway Jonas Gahr Stoere serikali yake imekuwa ikijaribu kuwasiliana na utawala wa Ethiopia ili kubainisha chanzo cha kutolewa amri hiyo lakini bila mafanikio .

Aidha ameelezea masikitiko yake juu ya uamuzi wa Ethiopia uliochukuliwa bila ya kuishauri Norway akisema hawana budi kujiandaa kuwaondoa wanadiplomasia wake sita katika ofisi zao za kibalozi mjini Adis Ababa.

Hata hivyo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Wahide Belay amesema hana habari juu ya kutolewa amri hiyo.