1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA.Serikali yawafuta kazi maafisa wake watatu wa ngazi za juu

20 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqy

Serikali ya Ethiopia imewafuta kazi maafisa wake watatu wa ngazi za juu katika jeshi la nchi hiyo.

Msemaji wa wizara ya ulinzi wa Ethiopia Dawit Assefa amesema kwamba maafisa hao ni meja generali Almeshet Degfe wa kikosi cha wanahewa, brigadia jenerali Kumeri Assefa wa jeshi la Ethiopia na Asamenew Tsgie wamepigwa marufuku kujihusisha na shughuli za ulinzi wa nchi hiyo.

Hata hivyo msemaji wa wizara ya ulinzi amesema hana taarifa zaidi juu ya uamuzi huo.