1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA.Katibu mkuu asisitiza kikosi cha amani kipelekwe Sudan

30 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWY
Mshabiki huyu wa Kichina anasubiri kwa hamu fainali
Mshabiki huyu wa Kichina anasubiri kwa hamu fainaliPicha: dpa - Bildfunk

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kwamba vizuizi visivyo na msingi ndio chanzo cha kuchelewesha misaada inayolenga kuwafikia wahanga wa umwagikaji damu katika jimbo la Darfur magharibi mwa Sudan.

Otton…..

Tangu nilipo chukuwa wadhfa wa ukatibu mkuu wa umoja wa mataifa nimelipa uzito mkubwa swala la Darfur….Uhusiano kati ya umoja wa Afrika na umoja wa mataifa ni wa muhimu zaidi katika swala hili…ni lazima tushirikiane katika kufanikisha kupelekwa kikosi cha ushirikiano cha jeshi la umoja wa Afrika na lile la umoja wa mataifa.

Pia katibu huyo mkuu wa umoja wa mataifa amekutana na rais Omar Hassan El Bashir wa Sudan pembeni mwa mkutano wa wakuu wa nchi na serikali za umoja wa nchi za Afrika AU unaoafanyika mjini Addis Ababa.

Hata hivyo habari zaidi zinafahamisha kuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa hakufanikiwa kupata jibu kamili kutoka kwa rais El Bashir juu ya kupelekwa wanajeshi 3000 wa umoja wa mataifa wa kulinda amani huko Darfur.

Wakati huo huo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesisitiza utengamano katika bara la Afrika akiiashiria Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kama mfano.