1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA : Raia wa kigeni 15 watekwa nyara

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCN3

Serikali nchini Ethiopia inaamini kwamba takriban raia wa kigeni 15 wametekwa nyara wakati wakisafiri katika eneo lilioko mbali nchini humo ambapo waasi wanaopigania kujitenga wamekuwa wakiendesha harakati zao.

Makundi mawili moja la Ufaransa lenye watalii kumi na jengine lenye raia wan chi tafauti yametoweka hapo Jumaatano wakati wakizuru jimbo kame la Afar lilioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Margaret Beckett amethibitisha kwamba wafanyakazi watano wa ubalozi wa Uingereza mjini Addis Ababa ni miongoni mwa watu hao wasiojulikana walipo.Taarifa zisizothibitishwa zimesema kwamba mojawapo ya kundi la utalii limewasiliana na kampuni yao ya utalii kwa njia ya simu ya satalaiti.

Katika kipidni cha hivi karibuni jimbo la Afar limekuwa eneo lililokumbwa na vitendo vya utekaji nyara.