1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA:Wakuu wa Afrika wavutana

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmL

Mkutano wa siku tatu wa wakuu wa nchi za afrika unafikia kilele leo hii, ambapo hapo jana ulikumbwa na tofauti juu ya njia za kuliimarisha bara hilo.

Viongozi hao wa afrika waligawanyika ama kushunghulikia na uundwaji wa serikali moja ya afrika, au kuimarisha kwanza taasisi za umoja huo wa afrika.

Rais Abdoulaye Wade wa Senegal; Omar Bongo wa Gabon na Mwai Kibaki wa Kenya ni miongoni mwa waliyoungana na kiongozi wa Libya Kanali Muhammar Gaddafi kutaka kuundwa kwa serikali ya shirikisho.

Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Umaru Ya radua wa Nigeria wao kwa upande wao walitaka kuimarishwa kwa taasisi za umoja wa afrika kabla ya kuundwa kwa serikali moja.