1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA: Rais wa Ujerumani Horst Köhler atoa wito kwa Umoja wa Ulaya kubadilisha mtazamo dhidi ya Afrika.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCag

Rais wa Ujerumani, Horst Köhler aliye ziarani nchini Ghana, ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kubadilisha mtazamo wake dhidi ya Afrika.

Rais Horst Köhler, ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha siku mbili kuhusu ushirikiano kati ya Ujerumani na Afrika, ameshutumu baadhi ya kampuni za Ujerumani zinazoshiriki ufisadi barani humo.

Rais Köhler alitoa wito kwa Ulaya kuendelea kununua bidhaa kutoka Afrika huku akizingatia zaidi athari mbaya ya sera za uvuvi barani Ulaya.

Kikao hicho kimeandaliwa kwa niaba ya mkakati wa ushirikiano na Afrika ulioanzishwa na Rais Horst Köhler.

Kikao cha kwanza kama hicho kiliandaliwa nchini Ujerumani mwezi Novemba mwaka elfu mbili na tano karibu na Bonn.