1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA : Mkutano wa Ujerumani na Afrika wafana

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaZ

Mkutano wa Ushirikiano kati ya Ujerumani na Afrika umemalizika katika mji mkuu wa Ghana Accra mwishoni mwa juma hili ambapo Rais wa Ghana John Kufour ameuelezea kuwa ulikuwa wa mafanikio makubwa sana.

Juhudi hizo za Rais Horst Köhler wa Ujerumani za kuwa na kikao cha siku mbili zimewapa fursa viongozi wa vijana takriban 50 kutoka Afrika na Ujerumani kukutana na viongozi wa ngazi ya juu katika siasa,utafiti na biashara na kujadili changamoto za jamii ya Afrika.

Katika mapendekezo yake ya mwisho kikao cha mkutano huo kimetowa wito wa kufanyika kwa mageuzi kabambe ya taasisi za kitaifa na kuzifanya ziwe wazi na ziwajibike.

Rais wa Ujerumani tayari amerudi Berlin baada ya kukamilisha ziara yake ya siku nne nchini Ghana.