1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA: Miaka 50 tangu Ghana kupata uhuru wake

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLz

Wananchi wa Ghana leo hii wanasherehekea mwaka wa 50 tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Uingereza.Ghana ilijitoa kwenye ukoloni wa Kingereza mwaka 1957 na hivyo kuanzisha mtindo ulioigwa na viongozi wengi barani Afrika.Sherehe za hii leo,zitahudhuriwa na viongozi kama Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini na waimbaji maarufu kama vile Stevie Wonder.Baadhi ya wananchi wa Ghana lakini wanakosoa mpango wa kutumia Dola milioni 20 kwa sherehe zitakazoendelea mwaka mzima.Wao wanasema,pesa hizo bora zingetumiwa kwa huduma za maji na nishati.Wakazi wa Ghana tangu miezi kadhaa wanakabiliwa na matatizo ya kukosa umeme.