1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA:Kiwanda cha mafuta chashambuliwa Bayelsa

7 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCln

Wapiganaji waliojihami kwa silaha wameshambulia kiwanda kimoja cha mafuta cha Agip katika jimbo la Bayelsa kwenye eneo la Niger Delta mapema hii leo na kuwateka wafanyikazi wawili wa kigeni.Hayo ni kwa mujibu wa kamishna wa Polisi katika jimbo hilo.

Kulingana na msemaji wa kiwanda hicho bado haijulikani kama utendaji kazi umeathirika.Kiwanda hicho kiko katika eneo la Brass ambako mapipa laki mbili ya mafuta yanazalishwa kwa siku.Utekaji wa wafanyikazi wa viwanda vya mafuta hutokea mara kwa mara katika eneo la Niger Delta.

Nigeria iliyo muuzaji wa nane mkubwa wa mafuta machafu ulimwenguni inapoteza zaidi ya mapipa nusu milioni ambayo ni humusi moja ya kiwango cha mafuta inayozalisha kwasababu ya wapiganaji hao .

Wapiganaji hao wanadai kuwa biahsra hiyo ya mafuta haiwanufaishi wakazi wa eneo hilo japo inaleta pato kubwa kwa serikali.Shambulio hilo linatokea juma moja kabla Nigeria kuandaa mkutano wa mawaziri wa shirika la mataifa yanayozalisha mafuta OPEC hapo Disemba 14.