1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA : Yar’Adua ashinda uchaguzi wa rais

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7l

Umaru Yar’Adua wa chama tawala cha People Demokratic ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais nchini Nigeria.

Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo yamempa gavana huyo mwenye umri wa miaka 56 wa jimbo la kaskazini la Katsina kura milioni 24.Mpinzani wake wa karibu kiongozi wa zamani wa kijeshi Muhammad Buhari amejipatia kura milioni sita na ameyakataa matokeo hayo kuwa ya udanganyifu mkubwa pamoja na kutowa wito kwa bunge kumshatki Rais Olusegun Obasanjo.

Msemaji wa upinzani Tom Ikimi amesema chama chake pamoja na vyama vyengine vitapinga matokeo ya uchaguzi huo mahkamani.

Umoja wa Ulaya na waangalizi wengine wa uchaguzi wameshutumu vikali jinsi uchaguzi huo ulivyofanyika. Kiongozi wa waangalizi hao wa Umoja wa Ulaya Max van den Berg amesema katika taarifa kwamba uchaguzi huo si wa kuaminika.

Takriban watu 200 inasemekana kuwa wameuwawa kutokana na ghasia za uchaguzi katika kipindi cha wiki moja iliopita.