ABUJA: Uchaguzi wa majimbo waendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 14.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA: Uchaguzi wa majimbo waendelea

Raia nchini Nigeria leo wanapiga kura kuwachaguwa magavana wa majimbo.

Kura ya leo inachukuliwa kuwa mtihani mkubwa kabla ya uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Hali ya usalama imeimarishwa kwa hofu kusije kukazuka machafuko yanayo dhaminiwa na makundi yanayo pingana.

Rais Olusegun Obasanjo amesema kwamba vurugu na wizi wa kura havitavumiliwa.

Taaarifa zaidi zinafahamisha kwamba katika jimbo la kusini lenye utajiri wa mafuta watu wenye silaha wamevamia kituo cha polisi katika mji wa Port Harcourt.

Polisi saba wameuwawa na wakati huo huo kituo hicho kimetiwa moto.

Wizara ya mambo ya ndani ya Nigeria imetoa amri ya kufungwa mipaka yake ya bara na pwani kwa saa kumi na mbili leo hii ili kuhakikisha zoezi hilo la uchaguzi linafanyika bila utata.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com