1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA : Nafasi ya makamo wa rais wa Nigeria iko wazi

24 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCgg

Rais Olesegun Obasanjo wa Nigeria hapo jana ametangaza nafasi ya makamo wake wa rais Atiku Abubakar kuwa wazi baada ya kuhamia chama cha upinzani kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika hapo mwakani.

Rais Obasanjo anatafuta mtu wa kujaza nafasi hiyo.

Abubakar alitumuliwa kwenye chama tawala cha PDP hapo Ijumaa baada ya kuasi na kuingia chama cha Action Congress cha AC ambapo kimechaguwa kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2007.

Ofisi ya makamo wa rais imesema kumuondowa Abubakar katika wadhifa huo kutakuwa sawa na kufanya mapinduzi na kwamba watalipinga jambo hilo mahkamani.

Katiba ya Nigeria inasema makamo wa rais anapaswa kuwa chama kimoja na rais wakati wa uchaguzi lakini haitaji suala la kuasi kwa kuhamia chama kengine pia inasema makamo wa rais anaweza tu kuondolewa kwa kujiuzulu,kifo au kwa kushtakiwa.