ABUJA: majeshi ya Nigeria yaua wapiganaji wa kiislamu 25 | Habari za Ulimwengu | DW | 19.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA: majeshi ya Nigeria yaua wapiganaji wa kiislamu 25

Majeshi ya Nigeria yamesema yamewaua wapiganaji wa kiislamu 25 katika mji wa Kano kaskazini mwa nchi hiyo.

Katika shambulio moja kubwa majeshi hayo yaliwazingira wapiganaji hao ambao hapo awali walikiteka kituo cha polisi na kuwaua polisi 13.

Wakati huo huo vyama vya upinzani vya Nigeria vinataka uchaguzi wa rais wa jumamosi ijayo uahirishwe kufuatia madai juu ya hitilafu zilizotokea katika uchaguzi wa majimbo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Usalama umeimarishwa nchini kote baada ya vifo vya watu 20 wakati wa uchaguzi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com