ABU-DHABI:Ujerumani kutoa mafunzo kwa wanajeshi 350 wa Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABU-DHABI:Ujerumani kutoa mafunzo kwa wanajeshi 350 wa Iraq

Maafisa wa Ujerumani,Iraq na Abu Dhabi wametiliana saini ya makubaliano yatakayohakikisha jeshi la Ujerumani linatoa mafunzo kwa kiasi cha wanajeshi 350 wa Iraq katika kipindi cha miaka kadhaa ijayo.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amesaini makubaliano hayo katika ziara yake kwenye eneo hilo la mashariki ya kati pamoja na wenzake wa Iraq na Abu Dhabi.Waziri wa uLinzi wa Ujerumani akiwa katika eneo hilo pia atawatembelea wanajeshi wa Ujerumani wanaopiga doria katika harakati za kuimarisha opresheni za kukabiliana na ugaidi katika eneo la bahari kwenye upembe wa Afrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com