ABU DHABI: Putin azuru jumuiya ya falme za kiarabu | Habari za Ulimwengu | DW | 11.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABU DHABI: Putin azuru jumuiya ya falme za kiarabu

Rais wa Urusi, Vladamir Putin, anazuru jumuiya ya falme za kiarabu. Akiongoza ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara raisf Putin amefanya mazungumzo kuhusu kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na jumuiya hiyo.

Katika ziara yake ya kwanza ya rais wa Urusi katika jumuiya ya falme za kiarabu, rais Vladamir Putin amekutana na rais wa jumuiya hiyo, Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahayan.

Viongozi hao walizungumzia juu ya kuimarisha uhusinao na kushuhudia kusainiwa kwa mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi. Mikataba hiyo inahusu ushirikiano katika kupambana na uhalifu, ulanguzi wa fedha, mashauriano ya kisiasa, elimu ya sayari na benki.

Aidha viongozi hao walijadili ufanisi uliopatikana katika mchakato wa kusaka amani ya Mashariki ya Kati na hali nchini Irak.

Sheikh Khalifa ameisifu Urusi kwa jukumu lake kama mshirika wa pande nne zinazodhamini juhudi za amani ya Mashariki ya Kati, zikiwemo pia Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.

Rais Putin aliwasili Abu Dhabi akitokea Australia ambako alihudhuria mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za Asia na Pacific, APEC.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com