1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abiria mmoja wa ndege ya United Airlines atolewa kwa nguvu

11 Aprili 2017

Video ya hivi karibuni iliyosambaa mitandaoni, inayomuonesha abiria wa ndege ya United Airlines akiburutwa na maafisa wa usalama kutoka ndani ya ndege imezua mijadala mbalimbali katika mitandao na vyombo vya habari.

https://p.dw.com/p/2b4Ef
USA United Airlines-Passagier wird aus einem Flugzeug gezogen in Chicago
Abiria wa ndege ya United Express akiburutwa na maasifa wa usalama Picha: picture-alliance/AP Photo/A. D. Bridges

 Katika video hiyo abiria mmoja aliburutwa na maafisa wa usalama huku akitoka damu.

Abiria huyo wakati wa tukio hilo alisikilikana akisema: Nataka kwenda nyumbani, nataka kwenda nyumbani.Akiomba abakishwe katika ndege hiyo ile aweze kuendelea na safari yake na kwenda nyumbani kwake.

Tukio hili linaweza kusababisha abiria wanaotaka kusafiri kufanya mgomo wa kuitumia ndege hiyo ya shirika la ndege la United Airlines, wakati wa kiangazi ambao shirika hili huwa na abiria wengi sana.

Kwa mji wa Chicago ni tatizo jengine la mahusiano na umma . Tayari mji huo unashitumiwa kuwa hauwezi kukabiliana na matatizo ya kihalifu yanayoyakumba baadhi ya mitaaa.

Tatizo hasa

Tatizo lilianza wakati shirila la United Airlines lilitaka kuchukua wafanyakazi  wanne waliotaka kwenda Louisviile. Jambo hili lilisababisha ndege kuzidi abiria na baadhi walitarajiwa kushuka. Katika kupunguza abiria United Airlines lilitaka watu wajitolee kushuka na walitaka kuwalipa abiria hao  dola 400, lakini hakuna aliyetaka kujitolea na baada yakuona kuwa hakuna aliyejitokeza, waliongeza kiwango cha pesa hadi kufikia dola 800, lakini pia hawakuwa na mafanikio. Baada ya kushindwa kupata abiria wa kujitolea shirika hilo la ndege liliamua  kuchakua hatua .

Ndege ya Shirika la United Airlines
Ndege ya Shirika la United AirlinesPicha: picture alliance/AP Photo/M. Evans

Waliamua wao watu wa kuwashusha. Watu watatu walishuka bila ya matatizo lakini mmoja alikataa, nakusema lazima aendelee na safari , kwa vile yeye alikuwa ni daktari na alikuwa lazima atibu mgojwa siku ya Jumatatu. Baada ya kushindwa kumshawishi abiri huyo maafisa wa usalama walianza kutumia nguvu, na kumvuta abiria huyo kutoka kiti chake na kuanza kumbutura hadi jee ya ndege.

Wakati maafisa hao wakifanya hivyo, abiria wengine katika video hiyo walikuwa wakisikika kusema, " Mungu wangu,mnafanya nini," "Mnavyofanya sivyo," "Tizameni mnavyofanya, mmempasua mdomo."

Abiria mmoja Tyler Bridges, alisema walijisikia kama walikuwa wakitekwanyara. "Tulikwama katika sehemu hiyo, hatukuweza  kufanya kitu chochote kama wasafiri. Unategemea tu shirika la ndege na uamuzi wao."

Baada ya tukio hilo hiyo jana, mkurugenzi wa shirika hilo Oscar Munoz aliandika barua na ilioneka katika barua hiyo kuwa alikuwa akiwawatetea wafanya kazi wa shirika lake kwa kusema mtu aliyeburutwa alikuwa akifanya fujo.

Sio kitu cha kushangaza mashirika ya ndege kuwapa abiri pesa ili waweze kutuo viti vyao kwa abiria wengine. Ikifikia hivo, shirika la ndege linatakiwa kulipa mara mbili zaidi ya bei ya mwanzo. Pia mashirika ya ndege yakiamua kufanya hivyo, yanatakiwa kufanya hivyo kwa maaandishi na kuelezea haki za abiria ambao wamekubali kushuka au kuuza viti vyao vya ndege.

Mwandishi: Najma Said/APE

Mhariri: Iddi Sessanga