Borussia Dortmund kuchuana na Nuremberg kesho. Dortmund itashinda ubingwa iwapo itashinda na Bayer Leverkusen ishindwe na Cologne.
Ghasia zimezuka kati ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina na viongozi wa Vyuo Vikuu kadhaa vya Marekani , huku masomo yakisitishwa na waandamanaji kukamatwa.
Tunisia imefanya mkutano wa kwanza wa ushauri na viongozi wa Algeria na Libya kwa matumaini ya kuanzisha muungano mpya wa eneo la Maghreb.
Shirika la afya ulimwenguni, WHO, limesema kuwa dawa ya majimaji ya kikohozi kwa watoto iliyogunduliwa kuwa na viambata vya sumu haipatikani tena katika nchi za Kiafrika ambako ilikuwa inauzwa.